Briefly

MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO VIONGOZI WA SERIKALI MKOANI RUVUMA Apr 14, 2026 News Update

Briefly
Registration, Insolvency and Trusteeship Agency Tanzaniapress_release
press_releaseTanzania·Registration, Insolvency and Trusteeship Agency Tanzania·Wire Summary

MEDIA CENTRE Mwanzo News Center April 14 2026 MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO VIONGOZI WA SERIKALI MKOANI RUVUMA News & Update ` Previous Next ?Kabidhi Wasii Mkuu Bw. Frank Kanyusi amewataka Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala na Maafisa Tarafa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa Usajili wa Ndoa za Kimila kwani inasaidia kutambua uhalali wa Ndoa na kulinda haki zao pamoja na watoto. ? ?Akizungumza wakati mafunzo hayo yaliyofanyika Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma Aprili 14, 2026 Bw. Kanyusi alisema viongozi hao wana nafasi kubwa ya kuwafikia wananchi moja kwa moja, hivyo amewaomba kutumia nafasi zao kutoa elimu hiyo zaidi kwa wananchi. ? ?Aidha, amesema uhifadhi wa Wosia ni muhimu kwa kuwa unasaidia kupunguza migogoro ya urithi na kuhakikisha mali za marehemu zinagawiwa kulingana na matakwa yake. ? ?Aliongeza kuwa RITA itaendelea kutoa mafunzo kwa viongozi wa Serikali katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara ili kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu huduma hizo, ?Mpaka sasa mikoa ambayo tayari imepatiwa mafunzo hayo ni pamoja na Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, Singida, Iringa, Manyara, Katavi, Kigoma, Tabora, Rukwa, Songwe na Mbeya.

AI Business Impact

How does this affect your business?

Get an AI analysis of this article grounded in your jurisdictions, practice areas, and any policy documents you've uploaded to Wansom.