Briefly

MHE. MBONI MHITA AFANYA ZIARA KUJIONEA MAFANIKIO YA KAPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA MKOANI SHINYANGA. May 19, 2026 News Update

Briefly
Registration, Insolvency and Trusteeship Agency Tanzaniapress_release
press_releaseTanzania·Registration, Insolvency and Trusteeship Agency Tanzania·Wire Summary

MEDIA CENTRE Mwanzo News Center May 19 2026 MHE. MBONI MHITA AFANYA ZIARA KUJIONEA MAFANIKIO YA KAPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA MKOANI SHINYANGA. News & Update ` Previous Next Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, ametembelea kuona huduma zitolewazo na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa wananchi kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inayoendelea katika Mkoa wa Shinyanga. Katika ziara yale leo Mei 19, 2026, Mhe. Mhita ameongozana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro pamoja na kamati ya ulinzi ya mkoa. Viongozi hao walipata fursa ya kushuhudia namna wananchi wanavyopatiwa huduma, hususani usajili wa vizazi na vifo, pamoja na elimu kuhusu umuhimu wa kuwa na nyaraka hizo katika kupata huduma za kijamii. Aidha, Mhe. Mhita alipokea taarifa fupi kuhusu utekelezaji wa huduma zinazotolewa na RITA tangu kuanza kwa kampeni hiyo. Taarifa hiyo imebainisha kuwa jumla ya wananchi 5,459 wamefikiwa na kupatiwa huduma za usajili pamoja na elimu kuhusu umuhimu wa nyaraka za utambulisho wa kisheria. Takwimu hizi zinaonesha mwitikio mkubwa wa wananchi na mafanikio ya kampeni katika kuwafikia watu wengi wenye uhitaji. Akizungumza machache katika ziara yake, Mhe. Mhita alieleza kuridhishwa na kazi inayofanywa na RITA pamoja na taasisi nyingine zinazoshiriki katika kampeni hiyo katika kuunga mkono juhudi za Serikali. Alisema huduma zinazotolewa zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi kwa kuwa zinawawezesha kupata nyaraka muhimu za utambulisho wa kisheria na kuongeza uelewa kuhusu haki zao za msingi hivyo kuwaasa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kujitokeza kwa wingi kutumia fursa ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ili kupata huduma mbalimbali zinazotolewa, kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anatambuliwa kisheria na anapata haki zake stahiki.

AI Business Impact

How does this affect your business?

Get an AI analysis of this article grounded in your jurisdictions, practice areas, and any policy documents you've uploaded to Wansom.

MHE. MBONI MHITA AFANYA ZIARA KUJIONEA MAFANIKIO YA KAPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA MKOANI SHINYANGA. May 19, 2026 News Update | Briefly | Briefly